Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Sijawahi kuwa na bima ya afya maishani

24924 Pic+diamond TanzaniaWeb

Thu, 1 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu kama 'Diamond Platnumz' amesema katika maisha yake hajawahi kuwa na bima ya afya.

Diamond ameyasema hayo leo Jumatano Oktoba 31, 2018 alipokuwa akikabidhiwa kadi za bima ya afya za Resolution kwa ajili yake na watoto wake watatu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi hizo, Diamond amesema katika maisha yake hajawahi kuwa na bima ya afya.

Hata hivyo, amesema baada ya kupatiwa elimu na kampuni hiyo ya bima, ameona kuna umuhimu wa kuwa nayo ukizingatia kuwa yeye ni msanii anaweza kupata ajali hata akiwa kwenye jukwaa.

Kadi alizopewa kwa ajili ya watoto wake Tiffah, Nillan na Dyllan, amesema  zitampunguzia gharama ya matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Resolution Insurance, Marryanne Mugo, amesema bima hiyo mbali na kupata huduma za matibabu katika hospitali mbalimbali nchini, pia itamwezesha Diamond kutibiwa nje ya nchi ikiwemo India na Uturuki endapo atapata rufaa za kimatibabu.

Wakati kwa wakazi wa Tandale, mkurugenzi huyo amesema jumla ya kaya 250 zitapatiwa kadi hizo na kila familia watoto wanne wataweza kutibiwa.

Alitaja thamani ya kadi hizo kuwa kila moja inagharimu Sh158,000 na wahusika watatakiwa kuzilipia kila mwaka.

Chanzo: mwananchi.co.tz