Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Platnumz “unataka niwe na vita na Wema ili iweje?”

2184 DSC 0354 660x400

Mon, 29 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Baada ya maneno kuzidi kuenea kwenye mitandao ya kijamii juu ya ukaribu ulionekana kati ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu usiku wa January 28,2018 katika utambulisho rasmi wa msanii Maromboso katika record label ya WCB na wengi kuanza kuhusisha ukaribu kama wamerudiana kimapenzi.

DiamondPlatnumz ameamua kuwatolea uvivu na kuchukua uamuzi wa kuandika kwenye ukurasa wake wa instagram kuhusu wale waliomsema kuwa amekosea kumualika Wema sepetu katika event hiyo, kwani wengi wanaamini baada ya Wema na Diamond kuacha hawawezi kuwa karibu.



“Wengi Hupenda kuona watu wakiwa wana Vita ama uhasimu usio na kichwa wala miguu… Eti utamsikia mtu anasema “Dogo Mi shabiki yako Mkubwa na nakukubali sana ila kitendo cha kumualika Wema Umeniuzi” kwaio we unataka mie niendelee kuwa na vita ama niwe na vita na Wema ili iweje? yani mie nikiwa na vita na Wema we unafaidika nini? na itanisaidia ama kusaidia nini kwenye Sanaa yetu?

“Huwezi kuwa shabiki yangu halaf unafurahia mie kuendelea kuwa na vita na mtu, tena vita ambayo imeshaisha…nina familia yangu Naipenda Naiheshimu na siwezi kuiacha… ila hio sio sababu ya kuwa na vita na watu…”

“Huu sio Muda wa kujenga chuki zisizo za msingi ni wakati wa wasanii kushirikiana na kwa pamoja kufanya kazi na kukuza sanaa zetu kwajili ya future ya wadogo na vizazi vyetu vijavyo… Shukran sana Mdam kwakuja usiku wa jana…Mwenyez Mungu akubariki na akujalie kila la kheri uliombalo…..”

Wema alivyomuita Diamond kwenye Stage (+Video)



 

 

Chanzo: millardayo.com