Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Platnumz kusafiri na walinzi 10, wasanii wajitokeza kwenda kigoma

90166 Diamond+pic Diamond Platnumz kusafiri na walinzi 10, wasanii wajitokeza kwenda kigoma

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hatimaye safari ya kwenda Kigoma inafanyika leo Jumamosi Desemba 28, 2019 kwenda kuadhimisha miaka kumi ya kimuziki ya msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz huku ulinzi wake ukiimalishwa.

Diamond ameamua kwenda kuadhimisha siku hiyo mkoani Kigoma ambako ndio kwao kwa lengo la kushukuru mashabiki zake kwa mchango wao kwenye muziki wake mpaka alipofikia kwa kuwa msanii mkubwa ndani na nje ya Tanzania.

Diamond aliyewasili stesheni ya Kamata Dar es Salaam leo Jumamosi Desemba 28, 2019 saa 12:00 asubuhi alikuwa ameongozana na walinzi 10.

Walinzi hao waliokuwa wamevaa nguo nyeusi walionekana wakiwa wamemzunguka Diamond wakati wote kuanzia anashuka kwenye gari lake hadi anakwenda kwenye treni ambako alipokewa na wenyeji wake ambao ni maofisa wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Diamond ambaye wakati wote alikuwa mwenye tabasamu, ameonyesha kushangazwa na idadi ya watu mbalimbali wakiwamo wasanii na waandishi wa habari waliojitokeza tayari kwa safari hiyo.

Diamond alipowasili alisababisha abiria waliokuwa wamekaa kwenye eneo hilo wakisubiri safari kumkimbilia na kumfuata mpaka alipofika geti la kwenda sehemu ya kupandia treni ambapo walinzi waliwazuia.

Juzi Alhamisi ya Desemba 26, 2019 Diamond alitangaza mabadiliko ya ratiba kwamba badala ya safari kuwa jana Ijumaa imesogezwa mbele hadi leo Jumamosi ili kutoa fursa ya watu wengi kushiriki hata waliokuwa safarini kurejea Dar es Salaam kuungana na hiyo safari.

Treni hiyo yenye mabehewa nane imeondoka saa 2:05 asubuhi safari licha ya awali taarifa kueleza safari ingeanza saa 12 asubuhi na wanaosafiri kutakiwa kufika saa 10 au 11 alfajiri.

Baadhi ya wasanii waliofika tayari kwa safari hiyo ni Jacline Wolper, Malkia Caren, Rayvanny, Dudu Baya ,Amber Lulu, Irene Uwoya, TID, Domo Kaya na Lavalava.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendelea katika safari hiyo

Chanzo: mwananchi.co.tz