Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Platnumz atoa pole waathirika ajali ya moto, aahidi kuwafuta machozi

FB IMG 1626008338106 Diamond Platnumz atoa pole waathirika ajali ya moto, aahidi kuwafuta machozi

Sun, 11 Jul 2021 Chanzo: dar24.com

Star wa muziki barani Afrika Diamond Platnumz ameoneshwa kuguswa na ajali za moto zilizotokea kwenye soko kuu la Kariakoo, Dar es salaam pamoja mkoa wa Morogoro

Diamond ametumia ukurasa wake wa instagram kwa kutoa taarifa yakuwa amepokea kwa masikitiko ajali hiyo iliyotokea Morogoro na sokoni Kariakoo

Aidha katika taarifa yake hiyo amesema kuwa kama kijana atashiriki katika hali na mali kurejesha faraja za ndugu waliopatwa na janga hilo

“Nimepokea kwa masikitiko ajali ya moto iliyotokea Morogoro na sokoni Kariakoo,mwenyezi mungu awatie nguvu wafanyabiashara wote pamoja na kila aliyeguswa na ajali hii ya moto,”

“Kama kijana wa kitanzania Niko tayari kushiriki katika hali na mali katika kurejesha faraja za ndugu zetu waliopatwa na tatizo hilo” ameandika Diamond Platnumz

Chanzo: dar24.com