Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Platnumz aanza na Pepsi baada ya kufunguliwa

38286 Diamondppic Diamond Platnumz aanza na Pepsi baada ya kufunguliwa

Fri, 25 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Siku moja baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kumfungulia staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz neema zimeanza kumiminika huku akijinasibu kuwa mwaka huu atapata kazi nyingi za ubalozi.

Diamond amesema Basata imemfungulia kipindi kizuri hivyo ana kila sababu ya kuishukuru Serikali kwa kumrudishia uhuru wake na amejipanga kufanya makubwa mwaka 2019.

Akizungumza wakati wa kutambulishwa kwa bidhaa ya Mkubwa Wao inayotolewa na kampuni ya SBC ambaye yeye ni balozi wake, Diamond amesema amejipanga kuzitendea haki kazi zote atakazozipata.

Amesema tangu alipoanza kufanya kazi na kampuni hiyo amejiona thamani yake kama msanii huku akizihamasisha kampuni nyingine kuendelea kuwatumia wasanii kama balozi.

“Nimefarijika kuwa balozi yaani hadi nasikia raha, nikipita barabarani kila kona naona picha yangu hadi bibie akija Tanzania anasema mpenzi wangu anafanya kazi,” anasema.

Kwa upande wake Meneja wa Mafunzo na Mradi wa SBC,  Rashid Chenja amesema bidhaa hiyo mpya imekuja kukidhi matakwa ya wateja wao.

“Mkubwa Wao ni kwa ajili ya Watanzania, tumeipa jina hilo kwa sababu ya ujazo mkubwa kuliko zote katika soko. Ujazo wake ni mililita 500 na itauzwa kwa Sh600,”amesema Chenja.



Chanzo: mwananchi.co.tz