Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Platnumz; Mwaka jana biashara, mwaka huu ni mziki mtamu

Diamond Yatapitaa Sdm.jpeg Diamond Platnumz

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, @Diamond Platnumz jana Ijumaa, Februari 3, 2023 aliachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Zuwena’ ikiwa ni moja ya Kuonyesha dhahiri kuwa Mwaka huu yupo zaidi kuwekeza nguvu zaidi kwenye kazi yake ya sanaa ya Muziki.

Ikumbukwe kuwa Mwezi Januari alianza kwa kuachia wimbo unaofahamika kama My Baby halafu ukafuatiwa na wimbo uitwao “YATAPITA” ambao umefanya poa sana katika majukwaa mbalimbali ya Muziki mtandaoni.

Kwa sasa anadhihirisha urejeo wake kamili wa kufanya makubwa zaidi katika huu mwaka yaani kwa mwezi wa kwanza na wa pili ameshachia jumla ya Nyimbo Tatu.

Msanii huyo mwaka jana japo alifanikiwa kuachia baadhi ya nyimbo na kumalizia na EP yake ya First Of All (FOA) bado sehemu kubwa ya nguvu yake aliiwekeza zaidi katika sekta ya Biashara ikijumuisha kufanyia promosheni zaidi kampuni inayojihusisha na michezo ya bahati nasibu ijulikanayo kama “WasafiBet” na Kuongeza zaidi masafa ya urushaji wa matangazo ya Wasafi Media hapa nchini katika maeneo ya mikoani kama vile alivyofanikiwa kufanya hivyo kwa jiji la Mbeya na Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live