Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Platnumz, Alikiba wamwambia haya Rais Samia

Mondi Pic Data Diamond Platnumz, Alikiba wamwambia haya Rais Samia

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Saa chache baa ya kuapishwa kwa Rais wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu, wasanii wa muziki wa Bongofleva, Diamond Platnumz, na Alikiba wampa maneno ya kutia nguvu Rais huyo.

Samia ameapishwa leo, Ijumaa Machi 19, 2021, Ikulu Dar es Salaam,akichukua nafasi ya aliyekuwa Rais wa Tanzania,  John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kushika kwake nafasi hiyo ya juu ya uongozi katika nchi, kunamfanya kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania na nchi za Afrika mashariki kuwa Rais.

Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wametumia kurasa zao kwenye mtandao wa Instagram, kumpa salamu za pongezi na kumuandika maneno yenye kuonyesha imani naye na kumpa moyo akiwemo, msanii Diamond Platnumz na Alikiba.

Wakati Alikiba akiandika maneno mafupi yaliyoambatana na picha ya Rais huyo na kusomeka’ “Allah akuongoze Mama, Mheshimiwa  Rais,’.

Related Walichosema mastaa wa kike baada ya Samia Suluhu kuapishwa kuwa Rais

Samia awashukuru wasanii waliotunga nyimbo kumuomboleza MagufuliDiamond yeye amenadika”Hongera sana mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.

“...Post na Comments za watu kuanzia mitandaoni mpaka majumbani, zinadhihirisha ni kiasi gani watu wanakupenda na wanaKuamini...na kukutakia kila la kheri katika kuendeleza mazuri aliyaanzisha Dr. John Pombe Magufuli na mengineyo mengi utayoyafanya,”.

Ukiacha Diamond na Alikiba pia yupo Shetta, meandika” Rasmi tunae mama, hongera Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Samia Suluhu Sassan. Mungu akakusimamie kwenye majukumu haya utuongoze vyema watanzania wote. Madam President.

Wakati msanii wa vichekesho, Lucas Mhuvile maarufu kwa jina la Joti ameandika” Hongera sana mama yetu, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tunakutakia kila la kheri katika uongozi wa kuliongoza Taifa la Tanzania.Hii ni historia isiyo futika kwa nchi Yetu.Mama wa Taifa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz