Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Platinumz atakavyobadilisha maisha ya wasanii

9559 Diamond+pic TZWeb

Wed, 20 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu  Diamond Platinumz amesema atahakikisha wasanii wanapata malipo mazuri kupitia Tamasha la Wasafi (Wasafi Festival), litakalofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 19 wakati wa uzinduzi wa chaneli ya Wasafi katika king’amuzi cha StarTimes, Diamond ambaye ni kiongozi wa WCB amesema wanajipanga kuona tamasha hilo linabadilisha maisha ya wasanii nchini.

Amesema tamasha hilo halina lengo la kuua wala kushindana na lingine lolote zaidi ya kuongeza nafasi kwa wasanii kupata nafasi ya kufanya kazi.

“Tamasha hili litakuwa likifanyika kila mwaka ila nitahakikisha kila msimu unapokwisha wasanii wanakwenda mapumziko nje ya nchi au wanaanzisha miradi kutokana na malipo mazuri nitakayowapa,” amesema Diamond.

Soma Zaidi: Diamond ‘anavyoichakaza’ thamani ya Zari, Hamisa

Amesema ili kufanikisha tamasha hilo, wanazungumza na wafadhili kuhakikisha wasanii wanapata fedha za kutosha zitakazobadilisha maisha.

“Tunaziomba kampuni zituunge mkono vijana kwa kufadhili tamasha hili,” amesema.

Diamond amesema kwa wafanyabiashara wataangalia namna wasanii na kampuni zitakazotoa ufadhili zitakavyonufaika.

Meneja wa WCB, Tale Tale maarufu Babu Tale amesema wamedhamiria kukuza sanaa na kuweka heshima kwa wasani.

Chanzo: mwananchi.co.tz