Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Nitafanya Shoo O2 Arena

Diamond O2 Arena Diamond Platnumz

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SUPASTAA wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amemesa kuwa ndoto yake nyingine kubwa ni kufanya shoo kwenye moja ya kumbi maarufu ulimwenguni, O2 Arena uliopo jijini London nchini Uingereza ambayo ni ndoto ya mastaa wengi wa muziki ulimwenguni ambao wamekuwa wakifanikiwa kutumbuiza katika ukumbi huo.

Diamond amedai kuwa shida sio kufanya shoo O2 Arena, lakini, je, ni Watanzania wangapi wataingia kwenye Arena hiyo, tofauti na wenzetu wenye utajiri wa watu kama Nigeria wanaoishi Ughaibuni.

Ikumbukwe kuwa, wasanii maarufu kutoka Nigeria akiwemo Burna Boy, Wizkid na Davido kwa nyakati tofauti wamefanya shoo katika Arena hiyo miezi michache iliyopita na kuweka rekodi ya kuujaza ukumbi huo wa aina yake.

Usiku wa jana, Jumatano, Machi 23, Diamond alikuwa akifanya Video Premier ya EP yake mpya ya FOA katika Ukumbi wa Cinemax Mlimani City, jambo ambalo halijawahi kufanywa na msanii yeyeote wa Bongo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live