Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Ningepewa Aslay nimsimamie, asingekuwa hapo!

Diamond Na Aslay Diamond: Ningepewa Aslay nimsimamie, asingekuwa alipo!

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bosi kubwa kutoka pale Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema, laity angepewa Aslay Isihaka amsimamie kimuziki, asingekuwa hapa alipo leo.

Diamond amefunguka hayo usiku wa kuamkia leo Agosti 17, 2022 alipokuwa kwenye uzinduzi wa albamu ya Love Sound Different ya msanii Elius Barnaba iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.

Alisema, wasanii wapo wengi ambao wana vipaji lakini tatizo lipo kwa wawekezaji wa huo muziki na ndio maana wapo wasanii wengi tu wakubwa lakini wanashindwa kufika kwenye kilele cha mafanikio.

“Mimi Aslay yule mnayemuona kama nikipewa nimsiamamie na kipaji alichonacho angekuwa mbali sana. Kaka yangu TID yule pale, angewekezewa hata Mil 100 tu ungeona asingekuwa hapa,” alisema Diamond.

Diamond alimaliza kwa kuiomba Serikali iangalie namna bora ya kuwekeza kwa wasanii na Basata kuweka sharia rafiki kwa wawekezaji kwani yapo malalamiko ya baadhi ya wawekezaji wanashindwa kuwekeza kutokana na kubanywa na sharia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live