Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Mbosso wasimulia mikufu yao ilivyokatika jukwaani

Diamond, Mbosso Wasimulia Mikufu Yao Ilivyokatika Jukwaani Diamond, Mbosso wasimulia mikufu yao ilivyokatika jukwaani

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mastaa wa Bongo nchini Tanzania Diamond Platnumz na Mbosso wamesimulia jinsi mikufu yao yenye vito vya dhahabu ilikatika walipokuwa wakitumbuiza wafuasi wao.

Diamond Platnumz kwa upande wake alisimulia;"Mkufu wangu ulikatika kipande kimoja wakati nlipokuwa nikitubuiza wafuasi wangu kwa kuwa ni wa gharama niliweza kuagiza wenye ujuzi waniuganishie."

Msanii huyu alidokeza kuwa mkufu wake ulisafirishwa hadi Uingereza kwa kituo kimoja ili kufanyiwa ukarabati kurudisha sehemu iliyokatika.

Nyota huyu wa Bongo alieleza kuwa mikufu yake ni ya gharama mno na kwa kawaida yeye huchagua maeneo ambayo atakayovaa wakati wa tamasha na ziara yake.

Kwa upande wa msanii Mbosso alieleza kuwa; "Mkufu wangu wenye mchoro wa kichwa changu ambao umeundwa kwa dhahabu ulikatika ila nashukuru kwa kuwa nilitumana kwa kituo hicho hicho Uingereza na ukarudishwa. "

Wawili hawa walisimulia hayo walipokuwa kwenye mahojiano ya moja kwa moja ndani ya basi walimokuwa wakisafiria.

Mikufu hiyo ya dhahabu yenye michoro ya vichwa vyao inatajwa kuwa za gharama mno.

Chanzo: Radio Jambo