Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Mama yangu hawezi kunipangia wa kumuoa

Diamond O2 Arena Diamond Platnumz

Sat, 16 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diamond Platnumz; ni chapa ya muziki nchini Tanzania ambaye baada ya kuwepo kwa tetesi kwamba mama yake, Mama Dangote huwa anampangia mwanamke wa kuoa, hatimaye ametolea ufafanuzi ishu hiyo.

Katika mahojiano na BBC Swahili, Diamond au Chibu anasema; “Kwanza wanamkosea sana mama yangu.

“Kwa umri wote huu (amezaliwa Oktoba 2, 1989 hivyo ana umri wa miaka 32), mama yangu hawezi kunipangia mtu wa kuoa.

“Hayo maisha yalishapita zamani sana ya mzazi kukupangia wewe umuoe nani au usimuoe nani, mama yangu hawezi kunipangia…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live