Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond: Lazima Ulimwengu Ututambue

Diamond Gh(2) Diamond: Lazima Ulimwengu Ututambue

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diamond Platnumz; ni supastaa wa Bongo Fleva ambaye anajisifia kwa kupandisha hadhi na viwango vya albam fupi (EP).

Akiwa kwenye hafla ya kuzindua video za nyimbo zilizopo kwenye EP yake ya First Of All (FOA) ndani ya Ukumbi wa Cinemax pale Mlimani City jijini Dar usiku wa kuamkia leo Alhamisi Machi 24, 2022, Simba anasema yeye pamoja na timu yake wametumia akili na pesa nyingi ili kuhakikisha EP hiyo inapata mapokezi mazuri hata katika mataifa ya kigeni.

Kwa kawaida EP haina sherehe nyingi ila Diamond aliandaa hafla tatu tofauti jambo linaloonesha kwamba ilikuwa na ukubwa wake.

Jamaa anasema hakufanya hivyo kuwapa presha wasanii wenzake, bali kuhakikisha kwamba wanamuziki hao wanajituma nje ya upeo wao kuachia kazi safi na zinazokubalika.

Diamond anasema kwamba atakuwa anafanya 'media tour' yake katika mataifa ya Marekani na Uingereza ili ulimwengu utambue kuwa kuna muziki unaitwa Bongo Fleva na unapatikana Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live