Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Harmonize wasalimiana Ikulu- Video

Diamond Harmonize (600 X 311) Diamond, Harmonize wasalimiana Ikulu- Video

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: Millard Ayo

Mastaa wa Bongofleva Diamond Platnumz na Harmonize jioni ya leo wamekutana Ikulu Jijini Dar es salaam na kusalimiana kwa kupeana mikono wakati wa futari iliyoandaliwa na Rais Samia na kuwaalika Watu mbalimbali wakiwemo Wasanii.

Harmonize alionekana kumfuata na kumsalimia Diamond aliyekua ameka pembeni ya Meneja Sallam ambapo katika sehemu ya maongezi yao, Harmonize alisikika akimwambia Diamond ‘nitakupigia kesho, pokea basi’.

Harmonize alisainiwa na Lebo ya WCB zaidi ya miaka tisa iliyopita lakini aliondoka kwenye lebo hiyo miaka zaidi ya minne iliyopita na toka hapo uhusiano wa wawili hao ulivunjika.

View this post on Instagram

A post shared by millardayo (@millardayo)

Chanzo: Millard Ayo