Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Harmonize na Ali Kiba kukutana tuzo za Afrimma

81664 Pic+tuzo Diamond, Harmonize na Ali Kiba kukutana tuzo za Afrimma

Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Wasanii wa Tanzania, Diamond Platnumz, Harmonize  na Ali Kiba watakutana katika  tuzo za Afrimma zitakazotolewa Oktoba 27, 2019 nchini Marekani.

Mtandao wa Afrimma unaonyesha kuwa Diamond na Ali Kiba  wanachuana katika vipengele viwili vya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki na mburudishaji bora.

Katika tuzo hizo Diamond atatoa burudani jukwaani sambamba na Ommy Dimpoz na Nandy. Wasanii  13 wa Tanzania wanawania tuzo katika vipengele mbalimbali.

Harmonize, Jux, Ommy Dimpoz na Rayvanny wameingia katika kipengele cha wasanii bora wa kiume Afrika Mashariki.

Vanessa na Nandy  wameingia  kwenye kipengele cha wasanii bora wa kike Afrika Mashariki.

Pia yupo Kenny ambaye ni mwongozaji wa video za muziki, watayarishaji wa muziki Kimambo na S2Kizzy;  Bujini na Rabbit Cre 255 ambao ni  wacheza shoo, DJ Ommy katika kipengele cha maDJ na mtangazaji wa redio Times,  Lil Ommy.

Pia Soma

Advertisement
Pia Aika na Nahreel wameingia katika kundi bora kupitia kundi lao la Navykenzo wakichuana na Sauti Sol wa nchini Kenya.

Chanzo: mwananchi.co.tz