Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Harmonize Kuvurugana Machi 4

Harmo+pic Diamond, Harmonize Kuvurugana Machi 4

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SUPASTAA wa Bongo Fleva, Harmonize ameamua kujivua ngozi mbele ya Diamond Platnumz, usiku huu amefunguka kwamba yupo studio anarekodi wimbo ambao utatoka March 4 mwaka huu, siku ambayo pia inafahamika Diamond Platnumz ataachia EP yake ya kwanza kwenye muziki.

Kwenye post yake hiyo hapa instagram, Konde Boy amejigamba kwamba wimbo huo utakuwa ndio wimbo bora wa mwaka huu.

Hii inakuwa ngoma ya tatu kwa mkali huyo ndani ya wiki Nne, ambapo alianza na ‘Mwaka Wangu’ kisha siku Kumi zilizopita aliachia REMIX ya ‘Omoyo’ wimbo wa Mchungaji Mwanamama Jane Misso.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live