Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Burna boy tayari wawasili tuzo za BET

Diamond Pic Data Diamond

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii kutoka Tanzania, Diamond Platnumz na yule wa kutoka nchini Nigeria Burna Boy, tayari wamewasili nchini Marekani kwa ajili ya kusubiri tukio la utoaji tuzo za ‘Best International Act’ BET.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa usiku wa kesho Jumapili majira ya saa tisa.

Kwa nyakati tofauti wasanii hao wameonekana kwenye video fupi huko mitandaoni wakiwa tayari wamewasili nchini Marekani na kupokelewa na wenyeji wao ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya shughuli hiyo.

Diamond kwa upande wake ameongozana na mmoja wa meneja wake, Hamis Tale, marufu kwa jina la Babu Tale.

Katika tuzo hizo mkali huyo wa kibao cha Waah!  anachuana na Wizkid, Burna Boy, Emicida, Headie, Aya Nakamura, Youssoupha na Young T & Bugsey katika kipengele cha kipengele ‘Best International Act’.

Endapo Diamond atanyakua tuzo hiyo,  atakuwa msanii wa pili kutoka Tanzania kuweka historia katika tuzo hizo,  baada ya Rayvanny ambaye mwaka  2017 alishinda katika kipengele cha 'Viewer’s Choice Best New International Act'  na kuwabwaga wasanii wengine akiwemo Dave, Amanda Black, Changmo, Daniel Caesar, Remi na Skip Marley.

Tuzo hizo na huandaliwa na kituo cha TV cha Black Entertainment Television huku  lengo la kuanzishwa kwake ikiwa ni kusherehekea mafanikio ya kazi za Wamarekani weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji, michezo na mengineo yahusiyo burudani.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz