Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Bob Junior waiteka treni, disko lapigwa usiku kucha

90253 Mond+pic Diamond, Bob Junior waiteka treni, disko lapigwa usiku kucha

Mon, 30 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ndoto ya Diamond Platnumz ya watu kucheza disco ndani ya treni aliyosafiri nayo imetimia usiku wa kumkia leo.

Hii na baada ya usiku mzima wa kuamkia leo Desemba 29, 2019 kukesha wakinywa na kucheza muziki ndani ya treni hiyo iliyotokea Jijini Dar es Salaam kwenda Kigoma mkoa alikozaliaa mama wa msanii huyo, Sandra.

Shughuli ya kucheza muziki wa mkesha ilianza saa 6:00 usiku baada ya watu kumaliza kula chakula ambapo kulikuwa na ubadilishwaji wa burudani mpaka jua lilipotoka asubuhi.

Kuna wakati zilipigwa nyimbo za wasanii mbalimbali wakiwemo wa wasafi na za nchi nyingine hususani Nigeria.

Watoa burudani waliokuwepo ndani ya behewa lililotengenezwa kwa ajili klabu walijua hasa nini watu wanachotaka kwani walipoona wamechoka nyimbo za kizungu na Bongofleva waliwawekea ngoma inayoita 'Kibao Kata'.

Kati ya watu waliokuwa kivutio usiku huo ni Diamond na Bob Junior, meneja wa kwanza wa msanii huyo na aliyetengeneza nyimbo nyingi katika albamu yake ya kwanza kumtoa kimuziki ya 'Nenda Kamwambie'.

Diamond na Bob walitumia zaidi ya saa mbili kucheza nyimbo zilizokuwa kwenye Albamu hiyo huku wakiimba kwa pamoja na kufarahi.

Pia wapambe wao hawakuwa nyuma kwa kuwasapoti huku wakiwashika vichwa na kuonyesha namna gani wamefurahi wawili hao kuwa pamoja tena.

Mchumba wake Diamond, Tanasha naye hakuwa mbali kwani walicheza naye muziki ambapo alikuwa akienda chumbani kumwangalia mtoto wao na kurudi.

Pia taa za usiku zilizokuwa zikiwaka ndani ya behewa hilo zilionekana kuwa kivutio kwa wakazi wanaoishi pembezoni mwa reli hiyo ambapo ilipofika kwenye baadhi ya stesheni walilifuata mmoja kwa moja behewa hilo huku wakimuita Diamond atoke kuwasalimia.

Wasanii wengine waliokuwepo usiku huo ni Irene Uwoya, TID, Umber Lulu, Queen Darleen, Lavalava na Rayvanny.

Burudani hizo ndani ya klabu ziliendelea hadi saa 1:30 asubuhi leo.

Chanzo: mwananchi.co.tz