Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond Atawakimbia Tena Kiba na Harmonize Kesho

Kiba Mondiz Diamond Atawakimbia Tena Kiba na Harmonize Kesho

Thu, 27 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KESHO Januari 28, 2022 tunategemea Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) litazindua rasmi tuzo za muziki Tanzania, kwa mujibu wa BASATA baadhi ya wasanii ambao wametajwa kuwepo kwenye tukio hilo ni Diamond, Alikiba, Harmonize.

Tujikumbushe kidogo, kwenye uzinduzi wa kampeni ya usafi Dar es Salaam, kampeni hiyo ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla.

Wasanii Alikiba, Harmonize na Diamond walialikwa na kutokea kumuunga mkono RC Makalla lakini kilichowashangaza watu Diamond ambaye naye ni mkazi wa dar es Salaam hakutokea, akatokomea mitini.

Haya tukio hili limejirudia, kesho Januari 28 tena wamealikwa na Basata, Je Diamond atatokea? Au atatokomea kusikojulikana kama kawaida yake?

Una ushauri gani kwa basata kama ikitokea Diamond hajatokea kwenye event hiyo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live