Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diamond, Alikiba, Harmonize wamejikosesha nafasi kumfurahisha Anko Magu

Kiba Pic Data Diamond, Alikiba, Harmonize wamejikosesha nafasi kumfurahisha Anko Magu

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NITAKWAMBIA Alikiba, Diamond na Harmonize hawapatani. Ukitaka nikupe ushahidi nitakwambia Seven Mosha, aliyekuwa meneja wa Alikiba miaka kadhaa nyuma aliwahi kukiri anafahamu msanii wake, yaani Alikiba hapatani na Diamond Platnumz.

Kwa kiasi fulani yeye na mameneja wa Diamond walijaribu kutaka kuwaweka sawa wasanii, lakini wahusika hawakuonyesha ushirikiano, ni kama Alikiba na Diamond hawakuwa wakitaka kumaliza tofauti zao.

Pia nitakukumbusha drama zinazondelea kati ya bosi wa lebo ya Konde Gang, msanii Hamronize na uongozi mzima wa WCB Wasafi, lebo ya Diamond Platnumz.

Mara wasimangane tena kwa kutajana majina kabisa huko Instagram, mara watukanane na kuitana majina yenye kuudhi kama vile Panya, Bonge, Njomba Nchumali na kadhalika.

Kubwa zaidi nitakwambia hata Anko Magu, enzi za uhai wake alikuwa na taarifa kwamba Diamond na Alikiba hawakuwa sawa, na pia alikuwa anafahamu kuwa Harmonize ‘alimkimbia’ Diamond na kusababisha pia kutokuwa na usawa.

Kwa ushahidi, nakukumbusha wakiwa Dodoma, Diamond, Alikiba na Hamronize walikaa meza moja, hilo ni jambo nadra sana kuona linatokea, na Anko Magu alipopanda jukwani kuhutubia hakuacha lipite hivi hivi, alisema;

“Nawashukuru sana wasanii, na mimi napenda kuona mna mshikamano na umoja, unapomuona Diamond na Alikiba wamekaa pamoja, wamekaa meza moja, hiyo inakuonyesha nguvu ya Chama cha Mapinduzi. Lakini pia unapomuona Harmonize aliyemkimbia Diamond, leo anaimba na kumsifia Diamond hadharani huo ndio utanzania ninaoutaka mimi.”

Hii ni sawa na kusema hayati Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa anatamani kuona wasanii hawatengani, wanafanya mambo yao kwa umoja, wanaweza kuwa wapinzani lakini sio maadui, alikuwa anatamani lile lililotokea pale Dodoma linadumu, alikuwa anatamani kukaa meza moja kwa Diamond, Harmonze na Alikiba kuwa chanzo cha umoja — lakini hapana, hilo limeshindikana mpaka mzee ametangulia mbele za haki.

Walikuwa na uwezo wa kumfurahisha mzee japo kidogo hata kwa kinafki katika kipindi hiki. Wangeweza kufanya mambo mengi ikiwemo kutengeneza wimbo wa pamoja, badala ya kila mtu kujifungua studio na timu yake na kutoa wimbo wake binafsi wangeweza kufanya kitu cha pamoja kwa ajili ya kumuaga mzee wao.

Hili halisemwi sana lakini mimi nashangazwa kusikia wimbo wa maombolezo ulioimbwa na wasanii A List wa Tanzania, lakini humo ndani humsikii Hamronize, humsikii Alikiba, ni kwamba hawajakizi vigezo au wao wako juu ya levo ya A list?

Sijui ni nani aliyefanya wakashindwa kushirikiana kwa namna hiyo, inaweza kuwa walioandaa wimbo huo hawakuwaita, inaweza kuwa waliokoseana waliitwa wakakataa, wala hakuna ulazima wakujua, lakini nadhani wamekosa nafasi moja nzuri ya kumfuruhisha tena Anko Magu kwa kumuonyesha Utanzania aliokuwa akiupenda.

Wangeimba nyimbo zao binafsi kama waliona kuna ulazima, lakini pia wangeshirikiana kwa pamoja kwenye nyakati hizi ambazo umoja unahitajika zaidi ya nyakati yoyote ile.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz