Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva aliyekuwa na Chino Kid afariki dunia

Chino Ajaliis (1) Dereva aliyekuwa na Chino Kid afariki dunia

Sun, 12 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Nabeel ambaye alikuwa dereva kwenye gari lililombeba mwanamuziki na mnenguaji, Isaya Mtambo maarufu ‘ChinoKid’ pamoja na wenzake, amefariki dunia kufuatia ajali ya gari iliyotokea siku ya jana.

Asubuhi ya leo Mtayarishaji wa muziki ‘Abbah Process’ amethibitisha taarifa hiyo ya masikitiko ambapo amesema wamempoteza mwanafamilia mwenzao ambaye amemtaja kwa jina la Nabeel.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Chino amepata majeraha sehemu ya kifua na sasa yupo hospitali ya Taifa Muhimbili huku baadhi ya ‘madansa’ wake wakidaiwa kuvunjika miguu.

Ajali hiyo ilitokea jana Jumamosi Novemba 11, 2023 eneo la Kabuku mkoani Tanga ambapo gari lao aina ya Toyota Alphard liligongana na lori la mafuta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live