Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Denzel: Hata sisi tuna hisia kama wanaume wengine

Denzel Msa Denzel: Hata sisi tuna hisia kama wanaume wengine

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkufunzi wa masuala ya utimamu wa miili, Denzel Trainer amesema kuwa kazi ya kufundisha gym hupaswi kutongoza wanawake ambao unawafundisha kwani kwa kufanya hivyo ni kupoteza watena na kujishushia heshima.

Denzel amefunguka hayo wakati akizungumzia kuhusu kazi yake hiyo na namna ambavyo wamekuwa wakikumbana na vishawishi vya aina mbalimbali sambamba na jamii inavyowachukulia walimu wa gym.

“Siwakingii kifua trainers, sisi pia ni wanaume, tuna hisia kama wanaume wengine, lakini linapokuja suala la kazi, hutakiwi kumtongoza mtu unayefanya naye kazi, siyo tu mwanafunzi wa pale lakini hata mtu mwingine.

“Mimi sijawahi kukutana na changamoto kama hiyo, lakini hata maofini kuna waume za watu wanatembea na wake zatu humo humo ofisini, sasa tunaweke kundi gani? Watu wanaoana ofisini humo humo, je, hao ni gym trainers? Na wao wana hisia kama walivyo watu wengine.

“Kwa gym trainers ni kosa kutembea na mke wa mtu, ni kosa kutembea na mwanafunzi wako na kama ukifanya hivyo huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako. Leo ukitongoza huyu, kesho yule, ukishamtoingoza hajalishi amekubali au amekataa, hawezi tena kukulipa ada na kazi yako itakufa.

“Mimi kama kuna mwanafunzi yeyote nimewahi kumfundisha akijitokeza akasema nimemtongoza, nipo tayari kumlipa,” amesema Denzel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live