Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dayoo na sababu ya kuitwa 'mangi'

DAYOOO Dayoo

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Dayoo amefunguka kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kwanini huwa anapenda kusema “NAITWA MANGI, NI MCHAGA TENA…” katika sehemu ya utangulizi wa nyimbo zake.

Hiyo imeelezwa baada ya Mtangazaji Abdallah Ambua (Dullah Planet) kugusia kuwa imetokea maranyingi yeye kuulizwa inamaanisha nini Dayo anapotumia aina hiyo ya maneno katika sehemu ya Sanaa yake.

Dayo alijibu kuwa “Mimi ni Mchaga kabisa kutokea Kilimanjaro” na kuongeza zaidi akasema kwamba amesoma na kukuwa kwa muda kidogo huko ila baada ya Bi mkubwa wake kuweka sawa baadhi ya mambo wakahamia Kigamboni hapa Jijini Dar es Salaam na ndiko alikoendelea na masomo baadae mishe nyingine kama hizi za muziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live