Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dayna Nyange mikononi mwa Davido

Dayna Pic Data Dayna Nyange mikononi mwa Davido

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Msanii wa Bongo Fleva, Dayna Nyange, anatarajia kuachia wimbo mpya aliomshirikisha staa kutoka nchini Nigeria, Davido. Hayo ameyaeleza leo Jumanne Mei  25, 2021 alipozungumza na Mwanaspoti, iliyotaka kujua ukweli kuhusu video ambazo zilikuwa zimesambaa mtandaoni zikimuonyesha akiwa studio na msanii huyo anayefanya vizuri nchini Nigeria. Katika maelezo yake Dayna alikiri kwamba ni kweli wameingia studio na Davido na kubainisha kwamba wimbo wao huo unatarajiwa kutoka rasmi Ijumaa ya wiki hii ya Mei 28 . Kutoka kwa wimbo huo kutamfanya Dayna kuwa msichana wa kwanza Bongo kutoa ngoma na Davido ambaye jina lake halisi ni David Adedeji Adeleke. Kwani kabla yake, msanii Diamond Platnumz miaka saba iliyopita aliwahi kufanya kolabo naye katika wimbo wake Number One kwa kuurudia na kuchangia kufungua milango kwa wasanii wa Nigeria kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa Tanzania. Wimbo huo hadi sasa umeshatazamwa zaidi ya mara milioni 44.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz