Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dayna Nyange awajibu kisomi wasiomsapoti

Elo Dayna Nyange awajibu kisomi wasiomsapoti

Mon, 14 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Msanii Dayna Nyange amesema hawezi kuwa-judge baadhi ya wasanii wa Tanzania ambao hawajaonyesha sapoti ya kushea wimbo wake aliofanya na staa wa muziki Afrika Davido kutoka nchini Nigeria.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumapili , 13th Jun , 2021 Picha ya msanii Dayna Nyange na Davido

Kupitia Mahakama Kuu ya Burudani 'Friday Night Live' ya East Africa TV ambayo inaruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 mpaka 5:00 usiku, Dayna Nyange amesema. 

"Wakati naachia kazi Nigeria sikuwa na-focus na hivi vitu ambavyo vingeweza kunifanya ni-lose concentration, Mimi ni binti wa kwanza East Africa nzima kufanya wimbo na Davido jambo langu limewashtua watu ni kazi kubwa, kwa ambao hawajaposti siwezi kuwajaji inawezekana walikuwa busy au hawakuwa na time nzuri".

Audio na video ya wimbo huo tayari imeshatoka na inaitwa Elo, pia Dayna Nyange anajiandaa kuja na EP yake ambayo maandalizi yamefanyika Nigeria.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.

Chanzo: eatv.tv