Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido yamkuta, afunguliwa mashtaka

Davido Afunguka Kupata Watoto Mapacha Davido yamkuta, afunguliwa mashtaka

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waandaaji wa tamasha la ‘Warri Again Concert’ wamemfungulia kesi ya madai ya N2.3 bilioni msanii kutoka nchini Nigeria Davido kwa madai ya kukiuka makubaliano ya kimkataba waliyoingia kati yao.

Tamasha hilo linalofanyika kila mwaka linalomilikiwa na aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini humo Amaju Pinnick, aliwasilisha kesi mbele ya mahakama kuu ya jimbo la Delta, huku mshitaki huyo akitaka Davido na 'lebo' yake kutoa fidia ya N2 bilioni.

Mshitaki huyo aliiomba mahakama kumtaka Davido kugharamia pesa ya mwanasheria na gharama za kufungua kesi pia anataka mahakama hiyo imuamuru mwanamuziki huyo kuomba msamaha kwenye mitandao yake yote ya kijamii na kwenye magazeti mawili yanayotoka kila siku kwa siku nne mfululizo.

Hii inakuja baada ya Davido kushindwa kufuata mkataba waliosaini na Amaju kuhusiana na tamasha hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live