Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido awapa onyo wanaosambaza picha zake za zamani

Davido Md.jpeg Davido awapa onyo wanaosambaza picha zake za zamani

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Davido kupitia mtandao wake X amewapa onyo wanaosambaza picha zake za zamani mtandaoni zikimuonesha akiwa na mkewe hospitali.

Picha hizo zimekuwa zikiambatanishwa na taarifa zinazodai kuwa amepata watoto mapacha hivi karibuni.

Hata hivyo, msanii huyo bado hajathibitisha au kukanusha uvumi huo wa kupata watoto mapacha na mkewe Chioma lakini ametoa onyo hilo kwa watu kuacha kutumia picha hizo za zamani.

Ikumbukwe wawili hao walimpoteza mtoto wao wa kwanza wakiume, aliyeitwa Ifeanyi, mwaka jana baada ya kudumbukia kwenye bwawa la kuogelea lililokuwa kwenye nyumba yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live