Mshindi wa Tuzo ya Nobel mwandishi wa Nigeria Wole Soyinka amemtetea nyota wa Afrobeats Davido kutokana na video ya muziki aliyoisambaza kwenye mitandao ya kijamii ambayo inadaiwa kuwakera Waislamu.
Sehemu moja ya video hiyo moja inasemekana kuwa ilionyesha wanaume waliovalia nguo nyeupe wakicheza mbele ya msikiti.
Hili lilizua shutuma kutoka kwa baadhi ya vijana waliokuwa na hasira huko Maiduguri, katika jiji lenye Waislamu wengi kaskazini-mashariki mwa Maiduguri kushambulia mabango ya Davido.
Video hiyo - kipande cha sekunde 45 kinachonadi wimbo mpya wa Logos Olori ambayo imesainiwa na lebo ya rekodi ya Davido - pia ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii.
Baadhi ya Waislamu mashuhuri walitaka kuombwa radhi, jambo lililomfanya mwimbaji huyo wa Nigeria kufuta video hiyo kwenye Instagram.
Lakini Prof Soyinka alikasirishwa na upinzani huo, ingawa alikiri kuwa hakuona video hiyo kwa sababu ilikuwa imetolewa.
Katika barua kwa mtandao wa habari ya Premium Times ya Nigeria, alisema:
"Kucheza dansi mbele ya msikiti hakufai kuchukuliwa kama kitendo cha uchochezi au kukera, bali inafaa kuwa kama uthibitisho wa umoja wa hisia za kiroho kwa mwanadamu.
Kuna kanuni, historia, haki na wajibu fulani wa ubunifu wa kisanii ambao haupaswi kuzuiwa kwa kigezo cha hisia.Kuna kanuni, historia, haki na wajibu fulani wa ubunifu wa kisanii ambao haupaswi kuzuiwa kwa kigezo cha hisia.
"Hakuna msamaha unaohitajika, hakuna anayepaswa kuombwa msamaha."Hakuna msamaha unaohitajika, hakuna anayepaswa kuombwa msamaha."