Mwimbaji Staa wa Nigeria Davido Adedeji Adeleke (Davido) jana amepewa heshima kubwa ya kutambulishwa kama Mgeni maalum katika Bunge la Seneti katika Jimbo la Georgia Nchini Marekani wakati mkutano wa Baraza kuu la Jimbo hilo ukiendelea.
Wawakilishi mbalimbali waliokuwepo kwenye ukumbi huo walisimama na kupiga makofi kama ishara ya heshima na kumkaribisha Mwimbaji huyu Staa ambaye pia ametambulishwa kama “Raia bora wa Jimbo la Georgia”
Utambulisho huu umepokelewa kwa heshima kubwa na Davido mwenyewe ambae alitumia ukurasa wake wa Instagram kuandika yafuatayo “Asubuhi ya leo nimehudhuria mkutano wa Baraza kuu la Jimbo la Georgia, Baraza la Wawakilishi la jimbo la Georgia na Seneti ya Jimbo la Georgia na kutambuliwa kama Raia Bora wa Georgia, Mungu ni mwema”
Davido ambaye Novemba 21 mwaka huu ametimiza umri wa miaka 31, alizaliwa Novemba 21 mwaka 1992 jijini Atlanta, Georgia nchini Marekani na kukulia Lagos Nigeria Baba yake akiwa Mfanyabiashara na Mama yake ambaye ni Marehemu kwa sasa (1963-2003) akiwa Mwalimu wa Chuo Kikuu