Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido aomba pesa kwa utani Twitter, ametumiwa zaidi ya Tsh. Milioni 542

Davido Olamide The Money Davido aomba hela kwa utani Twitter, atangaza kukusanya Tsh. Milioni 318

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji star wa Nigeria Davido ameweka salio la akaunti yake ya benki katika kurasa yake ya Twitter na kusema kuwa mashabiki wake wamenitumia fedha nyingi ndani ya saa moja mara baada ya kuwaomba wafanye hivyo.





"Kama unaujua kuwa kuna nyimbo niliimba na ikakupendeza .. nitumie pesa," Davido aliandika katika ukurasa wake wa tweeter kabla hajaanza kushirikisha kiasi ambacho wametumiwa.

Baadae aliandika kuwa amepata naira milioni 7 sawa na dola $16,000 ndani ya dakika 10, na kutania kuwa alikuwa amelenga kupata naira milioni 100 kwa sababu alikuwa anataka kulipia deni la gari alilochukua kwa mkopo aina ya Rolls-Royce.

Ujumbe wake wa mwisho kwa twitter unaonesha amepata naira milioni 97.

Davido ana wafuazi milioni 9.7 katika mtandao wa Twitter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live