Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido amzawadia ndinga kali Chioma siku ya harudi yao

Wife Chioma With All New GAC GN8 MPV Davido amzawadia ndinga kali Chioma siku ya harudi yao

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Kutoka nchini Nigeria, Davido amem-surprise mkewe, Chioma kwa kumpatia zawadi ya gari jipya la kifahari aina ya GAC Trumpchi GN8 MPV ya mwaka 2024 kwenye harusi yao inayofanyika huko Lagos nchini Nigeria.

Nyota huyo wa Afrobeats David Adeleke, maarufu Davido na mwanamuziki tajiri zaidi nchini Nigeria, amefunga ndoa na mpenzi wake Chioma Avril Rowland (aka Chef Chi).



Hii #ChiVido2024 inachukuliwa kuwa harusi kubwa zaidi kuwahi kuandaliwa nchini Nigeria, kwa kuwa inaalikwa tu kwa watu mashuhuri.

Jina la ukoo la Adeleke si geni kwa Wanigeria wengi; ni jina ambalo linajulikana katika tasnia nyingi nchini Nigeria.



GN8 yenye thamani ya dola $ 37,000 (sawa na Tsh milioni 97.5) ni toleo jipya lililoletwa hivi karibuni na GAC ​​Motor Nigeria, moja ya watengenezaji wakubwa wa magari wa China. Inaweza kulinganishwa na matoleo kama GS8 na GS7, ambayo tayari ni maarufu kwenye barabara za Nigeria kama SUV za juu za Uchina.

Je, Zawadi gani kubwa Unaweza kumzawadia mkeo au mumeo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live