Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido amnyoshea mikono Rema "Wewe ndio kinara wa Afrika kwa sasa"

Davido Rema Mtv Video Award 1200x720 Davido na Rema

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwimbaji wa Nigeria ‘Davido’,amempongeza msanii mwenzake ‘Rema’ kwa kufanikiwa kupenya kwenye anga ya muziki wa Amerika.

Remix ya ‘Rema’, “Calm Down” aliyomshirikisha Mrembo ‘Selena Gomez’ hivi karibuni imeweka rekodi ya kihistoria kuwa wimbo wa kwanza Barani Afrika na Nigeria kukaa mwaka mzima kwenye chati za Billboard ya Marekani.

Katika mahojiano ya hivi karibuni kwenye kipindi cha “The Kris Fade Show”,mkali wa Afrobeats ‘Davido’ amedai hakuwahi kufikiria kuwa msanii yeyote wa Nigeria angeingia kwenye chati.

Hata hivyo,ameshangazwa na jinsi ‘Rema’ kuendelea kusalia kwenye 5 Bora kwa wimbo wake katika kipindi cha miezi 8 iliyopita.

“Miaka iliyopita,Sikuwahi kufikiria kuwa msanii wa Nigeria angekuwa na rekodi 5 bora Amerika,Rema amefanya hivyo kwa miezi 8 iliyopita,bila kutikiswa,Yeye ni msanii bora,Nakumbuka nilikuwa Dubai miaka iliyopita na nikaona baadhi ya watu wakikoshwa na nyimbo zangu,Nilifurahi sana kuona hivyo,” amefunguka ‘Davido’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live