Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido ameninyima kolabo sababu ya bifu zetu - Harmonize

Harmo Na Mondi.png Davido ameninyima kolabo sababu ya bifu zetu - Harmonize

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Harmonize wakati akiwa kwenye interview na EATV amefunguka kuhusiana na Bifu lake na Diamond ambalo limemfanya Davido kukataa kolabo nayeye kupitia nyimbo ya Single again.

Ambapo kwa maelezo yake amesema kuwa wasanii wa Nigeria na Afrika Kusini wanasaidizana sana na wanapenda kuwasaidia wasanii wa Bongo lakini wakiangalia bifu za wasanii wa Bongo wanaogopa kuingia kwenye mtego wa kuwagawa mashabiki zao.

"Wakati nilivyokuwa USA Davido alinitafuta na kuniomba tufanye Remix ya 'Single Again', mimi ilinibidi nimtumie kipande changu ili naye aingize kipande chake, lakini cha kushangaza mpaka leo Davido amenikaushia na hata akunijibu.

"Hivyo sababu ya yote ni bifu letu kwa sababu alihisi kama akifanya kolabo na mimi wenda itakuwa chuki kwa wengine, alafu Nigeria waoo mtu akikosea huwa wanaumia na kusaidiana lakini Bongo mtu akikosea anasemwa uku anatukanwa," amesema Harmonize.

Je, una kipi cha kumshauri Harmonize baada ya kukataliwa Kolabo na Davido?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live