Imeripotiwa kuwa Staa wa muziki Davido na mpenzi wake Chioma wamefunga ndoa ya kitamaduni kwa siri.
Haya yanajiri wiki chache baada ya wanandoa hao kumpoteza mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka mitatu, Ifeanyi ambaye alizama kwenye Swimmingi pool katika jumba la kifahari la msanii huyo katika kisiwa cha Banana huko Lagos na kufariki.
Harusi hiyo ya kitamaduni, ambayo ilihudhuriwa na familia na marafiki wachache inasemekana ilifanyika tarehe 6 Novemba katika nyumba ya babake Davido, bila kamera kuruhusiwa na Mahari ya Chioma ililipwa kikamilifu.
Ndoa hiyo ilikuwa ni lazima ifungwe ili Mtoto wao Ifeanyi ambae alifariki aweze kuzikwa kama mmoja wa familia ya Davido kulingana na tamaduni za jamii ya Igbo.