Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido, Burna Boy kumekucha tena!

Burna Boy Davido.jpeg Burna Boy na Davido

Sat, 14 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mei 13, 2022 ukiachana na headlines za msanii maarufu duniani, Kendrick Lamar kudropisha Albamu yake ya Molare & The Steppers na mitandao kama Apple Music na Spotify ku-crash kutokana na wingi wa watu kui-stream albamu hiyo...

Back to Africa ambapo tarehe hii pia, wasanii maarufu Davido pamoja na Burna Boy wapo kwenye macho ya mashabiki kuona nani atamgalagaza mwenzie kwenye projects zao ambazo wameachia pamoja, Davido akiwa na Stand Strong na Burna Boy akiwa na Last Last.

Masaa kadhaa nyuma, Davido alifanikiwa kushika No. 1 kwenye Apple Music Nigeria (Top songs) kitendo kilicho fanya aweke Insta story kuwa anaitwa 001,ishu ambayo kwa mashabiki imeonekana kama ni kijembe kwa Burna Boy ambaye alikuwa No.3, (sasa No. 2).

Mitandaoni Mashabiki wa Burna Boy na Wizkid wanaamini ni suala la muda tu, Burna Boy anaenda kuichukua No.1

Chanzo: www.tanzaniaweb.live