Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Davido, A.Y (Comedian) kuburuzwa mahakamani

1288 Dav T Horz 740x313 TZW

Mon, 15 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido huenda akaburuzwa mahakamani endapo upepelezi ukikamilika kuwa alikwepa kulipa kodi kwenye serikali ya jimbo la Lagos baada ya kufanya tamasha kubwa la funga mwaka la 30 Bilion Concert.

Davido na A.Y (Comedian)

Mamlaka ya mapato jijini Lagos (LIRS)  imesema Davido amekuwa akikwepa kodi kwa miaka miwili mfululizo na kusingizia kuwa analipa kodi zote katika jimbo la Osun ambako ndiko anakoishi kitu ambacho mamlaka hiyo imesema ni kinyume na sheria za kodi.

Mamlaka hiyo imesema inamtaka Davido aoneshe risiti za kodi alizolipa kwenye jimbo la Lagos baada ya tamasha lake la 30 Bilion Concert ambalo lilifanyika katika jimbo hilo huku likiahidi kumchukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kumpeleka mahakamani.

Davido amesaini dili kubwa na Sony Music Entertainments amesaini dili za matangazo na makampuni makubwa hivyo tunahitaji kuona nyaraka zake za kodi aliyolipa kwenye mikataba yake yote,“imeeleza taarifa hiyo ya (LIRS) huku ikihoji tamasha lake la 30 Bilion Concert ambalo aliutangazia umma kuwa ameingiza kiasi cha Naira Milioni 500 (Tsh bilioni 3).

Davido alifanya tamasha la 30 Bilion Concert na alitangaza kuwa aliingiza kiasi cha Naira milioni 500 tunataka pia kujua kama alilipa kodi na atuoneshe nyaraka za (LIRS) jinsi alivyolipa kodi kabla ya kumchukulia hatua

Hata hivyo Meneja wa Davido, Asa Asika amethibitisha kupokea taarifa hizo lakini amesema atatolea maelezo baadae baada ya kukamilisha ripoti ya kodi.

Kwa upande mwingine mamlaka hiyo imemtaka pia mchekeshaji maarufu nchini Nigeria A.Y naye apeleke nyaraka za malipo ya kodi ya tamasha lake alilofanya mwishoni mwa mwaka jana ambapo naye alitangaza kuwa ameingiza kiasi cha hela kama Davido huku akijijitetea kuwa yeye kodi zote analipa katika jimbo la Ondo ambako ndiko anakotoka.

“AY too said the same thing. The comedian claimed to be paying his taxes to Ondo State, where he hails from. It seems these celebrities don’t understand that the tax law stipulates that you must pay your tax to your state of residence.

“Anyway, we are already in court. Others will soon appear in court if they don’t obey the state tax law. You can’t be making money in Lagos and refuse to pay tax.”

Chanzo: bongo5.com