Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Darleen: Sijui kama bado nipo naye

Queen Darleen Queen Darling

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki Mwanahawa Abdul Juma almaarufu Queen Darleen amefunguka kuhusu ndoa yake na mfanyibiashara Isihaka Mtoro.

Darleen ambaye ni dada mkubwa wa Diamond Platnumz anakiri kuwa hana uhakika kama bado yuko kwenye ndoa au tayari ameachika.

Anasema kuwa bado anampenda mume wake na huwa wanawasiliana mara kwa mara. “Kiukweli mpaka sasa sijijui. Sijui kama niko kwenye ndoa au siko kwenye ndoa. Nampenda sana mume wangu. Popote alipo ajue kwamba nampenda sana. Yeye ndiye anajua kama niko naye au siko naye," anasema Darleen kwa huzuni.

Kauli hiyo ya Darleen inakuja miezi kadhaa ya tetesi kuwa wanga wamepita na ndoa yake baada ya kujaaliwa mtoto mmoja na jamaa huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live