Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Darassa: Tumuenzi Magufuli kwa kufanya kazi

9d58fa25365a61e3642e4ae8915725ad Darassa: Tumuenzi Magufuli kwa kufanya kazi

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Sharif Thabeet ‘Darassa’ amehimiza Watanzania kumuezi Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, John Magufuli kwa kile alichokuwa akisisitiza watu kufanya kazi kwa bidii.

Akizungumza Dar es Salaam Darassa alisema watu wakijituma na kufanya kile, ambacho Rais Magufuli alikitaka basi wanaweza kufanikiwa katika maisha.

“Mwito wangu kwa Watanzania hayati Rais wetu alikuwa anataka watu wafanye kazi, wajitume kwa hiyo tunaweza kuchukua vitu vyake na kwenda mbele, tumuenzi na kumfanya aishi milele,”alisema.

Rais huyo aliyepita alifariki dunia Machi 17, mwaka huu Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao Chato wiki ijayo.

Tayari ya nafasi ya kiongozi huyo imechukuliwa na aliyekuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu baada ya kuapishwa juzi kushika wadhifa huo kwa ajili ya kusimamia shughuli za kitaifa.

Kufuatia kifo hicho ilitangazwa siku 21 za maombolezo hivyo, hakutakuwa na shughuli zozote za burudani hadi zitakapomalizika taratibu zote za msiba.

Chanzo: www.habarileo.co.tz