Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dame Dash amaliza bifu lake na Jay Z

Dame Dash Jay Z Lawsuit 1200x675 Dame Dash amaliza bifu lake na Jay Z

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dame Dash ambaye alikuwa akishirikiana na Jay Z kuimiliki ‘lebo’ ya ‘Rock A Fella’, ameweka wazi kuwa yuko tayari kufanya mazungumzo na Jay Z ili wamalize tofauti zao na kurudisha nguvu katika ‘lebo’ hiyo.

Kufuatia mahojiano yake na ‘The CEO Show’, Dash ameweka wazi kuwa ugomvi wake na Jay ulikuwa ni kumuweka mbali msanii huyo na watu wake wa karibu wanaomtumia vibaya huku aliweka wazi kuwa lengo lake lilikuwa kumuokoa msanii huyo

Kufuatia mazungumzo hayo Dash amedai kuwa hana kinyongo na Jay Z na yupo tayari kufanya mazungumzo nae huku akieleza kinacho wakwamisha ni kuwa kwa sasa kila mtu yuko busy na mambo yake.

Awali Dame na Jay-Z walikuwa wakifanya kazi pamoja na baadaye waliingia kwenye mgogoro wa kibiashara uliofanya wawili hao kutengana huku Dash akaamua kuisusa Rock-a-fella .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live