Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktar: Ommy Dimpoz anaweza kuendelea na muziki

14537 Dimpoz+pic TanzaniaWeb

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya koo, masikio na pua katika Chuo Kikuu cha Afya Shirikishi Muhimbili (Muhas), Godlove Mfuko amesema mwanamuziki Ommy Dimpoz anaweza kuendelea na muziki iwapo tu tatizo lake lilikuwa katika mfumo wa chakula pekee.

Dimpoz alifanyiwa upasuaji wa koo takribani miezi mitatu iliyopita baada ya kupata tatizo la kushindwa kumeza chakula.

Katika mahojiano na MCL Digital, jana Agosti 28, 2018 alipoulizwa iwapo mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa koo anaweza kuendelea na kazi ya kuimba, amebainisha kuwa koo la chakula halina uhusiano na  la sauti ambalo kazi yake nyingine ni kupitisha hewa.

“Ugonjwa huu unaweza kuziba sehemu tatu, kwenye koo mpaka kifua au mpaka tumbo, kwa hivyo mara nyingi kama mgonjwa anashindwa kumeza chakula huwa hana matatizo katika koo la sauti,” amesema.

Dk Mfuko anafafanua kwamba koo la sauti lina kazi mbili kupumua na kutoa sauti.

“Mgonjwa akiwa na shida ya koo la chakula dalili huwa hazitokei mapema, mara nyingi anakuja hospitali akiwa na dalili za kushindwa kumeza lakini katika hatua za mwishoni na kama ni saratani basi huwa imeshafika hatua za pili au tatu tofauti na tatizo katika upande wa sauti,” amesema.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa iwapo mtu atakuwa na matumizi mabaya ya sauti unaweza kupata shida.

“Tatizo kama hili wanapata sana walimu na wahubiri anaweza kupata tatizo hilo likaathiri koo lake, tiba yake haina uhusiano na tiba ya saratani,” amesema.

Soma Zaidi:

Daktari azungumzia ugonjwa unaomsumbua Ommy Dimpoz

Chanzo: mwananchi.co.tz