Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dah ya Manara na Zaylissa yamuongezea maokoto Nandy

Nandy Manara Zay (1).jpeg Dah ya Manara na Zaylissa yamuongezea maokoto Nandy

Sun, 11 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuachia ngoma ya 'Dah' maalumu kwa ajili ya kusherehesha mahusiano ya Haji Manara na Zaylisa, Mwanadada Faustina Charles 'Nady' amesema wimbo huo umeendelea kuwa mkubwa.

Iko hivi; Staa huyo wa wimbo huo ambao upo nafasi ya kwanza kwenye nyimbo zinazosikilizwa sana Tanzania kwa sasa, amesema ameendelea kupokea simu nyingi za kufanyiwa remix kwa wimbo huo. Wimbo huo tayari una remix ya King wa Bongo Fleva, Alikiba.

Wakati wawili hao wakiendelea kuteka soko la mapenzi na kibao hicho, staa kutoka Marekani Usher Raymond naye ameomba kuingiza mashairi yake.

Nandy ameshare chati zake na staa huyo wa Marekani akiomba kuweka mashairi yake wakati kazi hiyo ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki.

Hata hivyo, staa huyo ametoa nafasi kwa wasanii na mashabiki kuimba wimbo huo na kumtumia, atakayeshinda atajishindia shilingi milioni moja.

Amesema tayari rapa Stamina ametuma mashairi yake akichana na kuongeza ubora wa kazi hiyo ambayo ndani ya wiki moja tayari imetazamwa na watu milioni 3.1 kwenye mtandao wa You Tube.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live