Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daddy Yankee ndiyo basi tena

Daddy Yankee  Ad Daddy Yankee

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Daddy Yankee ametangaza rasmi kuachana na Muziki wa Reggaeton (wa kidunia) na kukimbilia kukabidhi maisha yake kwa Yesu Kristo.

Akizungumza kwenye video ambayo ameiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, amesema kwamba haoni aibu kuuambia ulimwengu kuwa Yesu anaishi ndani yake.

Daddy Yankee mwenye umri wa miaka 46 amesema anatumai atabadili jina lake la usanii tayari kwa kuanza kumtumikia bwana ambapo atatumia jina lake la kuzaliwa, “Ramón Ayala.”

Yankee amewahi kutamba na ngoma ya “Gasolina” “Dura” “Limbo” pamoja na hit ya muda wote ya “Despacito” aliyoshirikishwa na Luis Fonsi mwaka 2017.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live