Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dada wa 'Make Up': Niliyoyasema kuhusu kiba nilipangwa

Dada Kiba Kiba na Lulu

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo anayejulikana kwa jina la #Lulu amemuomba msamaha supastaa wa Bongo Fleva, Alikiba baada ya kusema mameno ya kumchafua katika mtandao ya kijamii.

Akifanyiwa mahojiano na moja ya online media hapa Bongo, Lulu alieleza kuwa yeye ndiyo aliyempaka Alikiba 'Make Up' wakati wa kuandaa video yake ya mahaba huku akidai kuwa Kiba alimlipa kiasi cha Tsh 20,000 tu.

Katika mahojiano hayo, Lulu aliongeza kuwa Alikiba ni bahili na hana hela ya kumlipa ndiyo maana alimpaka make up vibaya.

Baada ya mahojiano hayo kusambaa mitamndaoni, Uongozi wa King Kiuba ulitoa maelezo kuwa kauli hiyo ni ya uongo na yenye nia ya kuchafua jina, brand na heshima aliyojiwekea msanii huyo kwenye jamii.

Uongozi wa Kiba ulienda mbele zaidi na kusema kuwa wanajipanga kwendA mahakamani kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika katika kumchafua huku akiwaomba radhi mashabiki zake kwa usumbufu uliojitokeza.

Baada ya barua hiyo, Lulu amerudi tena na kueleza kuwa kuwa alichokizungumza kwenye mahojiano yake ni uongo na hajawahi kuoanana na Alikiba na maneno aliyoyaongea alipangwa (alielekezwa) na waliomhoji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live