Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Dada wa Dulla Makabila: Ningekufa kwa kudanga mie!

Aminaa Amina Vikoba.

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa maigizo nchini, maarufu kama Amina Vikoba ambaye ni dada wa msanii wa Singeli, Dulla Makabila amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumfanya kuwa staa akiwa mkubwa kwani angepata umaarufu huo akiwa mdogo huenda angekufa mapema.

Akizungumza kuhusu maisha yake, Amina amesema; "Nimeanza kuigiza kitambo sana, lakini kila jambo na wakati wake na huu ndio wakati wangu, Mwenyezi Mungu labda alinipunguza akajua huyu nikimtoa bado msichana mbichi maziwa yapo juu huyu atakufa,.

"Kwa hiyo Mungu kanitoa sasa hivi kidogo ziwa liko saa tatu na nusu, saa kumi 12 kamili, kwa hiyo sijutii hilo nalishukuru kwa sababu watu wameanza kuona kazi zangu na wameona ninavyofanya vizuri lakini nina familia yangu.

"Nina mume wangu, nina watoto watano kwa hiyo inanipa heshima hata kama mtu akinifuata DM akinitikisa na pesa, nitazitamani pesa lakini lazima nitamfikiria mume wangu jinsi anavyonitunza nitaogopa.

"Sasa ningetoka wakati ule nikiwa ziwa saa sita ingekuwaje? Kwa hiyo Mungu ananipenda maana kwa jinsi ninavyopenda pesa ningekufa kwa kudanga na uzuri huu nisingeziacha.

"Hapa nilipo nina watoto watano ni mama mkubwa mwenye age yake lakini bado naita, we pata picha nilipokuwa na miaka 18 nilikuwaje? Kwa kweli ningekufa, na kikubwa ambacho kingeniua ni mambo ya pesa.

"Michezo ya pesa kwa sababu nisingetaka kuwa na mume ningetaka kudanga, ningejidangisha-dangisha ilimradi nipate maokoto kila sehemu, kwa hiyo hayo ndiyo yangeniua,"- Amina Vikoba dada wa Dulla Makabila.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live