Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DUDU BAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTUMIA LUGHA CHAFU MTANDAONI

DUDU?fit=800%2C445 DUDU BAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTUMIA LUGHA CHAFU MTANDAONI

Thu, 21 Jan 2021 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mwanamuzi wa bongofreva Godfrey Tumaini maarufu Kama Dudubaya (41) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni kwa kosa la kutumia lugha chafu mtandaoni.

Dudu baya amesomewa hati ya Mashtaka na Wakili wa Serikali Hilda Katto mbele ya Hakimu Mkazi Ester Mwakalinga ambapo Wakili amedai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 11, mwaka 2020 akiwa nchini Tanzania

 “ mshtakiwa Dudubaya aliandika lugha ya matusi kwa Joseph Kusaga katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuisambaza ”

Mshtakiwa alikana kutenda kosa, kwa upande wa Jamhuri Wakili amedai upelelezi umekamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe kwa ajili ya kusikilizwa.

Dudubaya yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaokidhi vigezo vya Mahakama sambamba na kutia saini bondi ya sh. milioni 2. na kesi itasikilizwa Januari 28, 2021.

Chanzo: zanzibar24.co.tz