Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DStv yaja na chaneli mpya ya kiafrika 'Honey'

83f7c4962aa19b28b7651eb2494a8490 DStv yaja na chaneli mpya ya kiafrika 'Honey'

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Burudani ndani ya DStv inazidi kukolea baada ya kuanza kuonesha chaneli maarufu ya maisha halisi ya kiafrika ijulikanayo kama HONEY inayoanza kupasua mawimbi leo Februari 15, 2021.

Chaneli hii inayoonekana DSttv 173 imesheheni burudani huku ukiweza kushuhudia maisha ya watu mashuhuri wa Kiafrika ikiwa kwenye uhalisia wake na kutengenezwa na waandaji wenye vipaji. Hapa utashuhudia mapishi, mahusioano, harusi pamoja na maudhui mengine kutoka pande zote za dunia.

Kulingana na uwepo wa wanadada mashuhuri kama Pearl Umeh (Nigeria), Patricia Kihoro, Foi Wambui (Kenya), Anele Mdoda, Mbali Nkosi na Anele Zondo (Africa Kusini), hakika chaneli hii itakuwa bora na yenye mvuto muda wote.

DStv imekuwa kitovu cha burudani kwa wapenzi na watazamaji wa televisheni na kila wakati imekuwa mstari wa mbele kuweka chaneli nyingi za kiafrika na hivyo kupanua wigo wa kazi za kiafrika kuonekana zaidi na hivyo kuchangia kikamilifu katika kuhakikisha kuwa maudhui ya kiafrika yanapata nafasi kubwa.

Chaneli ya Honey ina vipindi vingi na vyakuvutia ikiwemo;

Pastors’ wives

Ndani na kipindi hiki utakutana na wanawake walioweza kuongoza familia kwa kupitia misingi ya dini. Mtengenezaji wa kipindi hiki ni Sonia Mbele ambaye pia alitengeneza The Real Housewives of Joburg na ameweza kutengeza Postor’s Wives kwa mwenenedo wa dunia nzima na jinsi wanavyoweza kuongoza familia na jumuiya za makanisa yao kwa ubora.

Love swap

Hii ni tamthilia yenye uhalilisia inyoonyeshea changamoto za mahusiono ambapo wapenzi wanabadilishana wapenzi wao kwa kupitia chakula cha nyumbani cha usiku. Kila kipindi kitakuwa kinaelezea maoni waliyonayo na mambo waliyojifunza kutoka kwa wapenzi waliokutana nao siku hiyo.

Making the menu

Ndani ya kipindi hiki, wanakutana wanablogu wa chakula wawili na kutengeneza chakula kisha mtu maarufu atahitaji kuonja na baadae mmiliki wa mgahawa ataamua ni chakula gani akiongeze kwenye mpango wake wa chakula yaani Menu.

Yes! Ndio! Beeni!

Patricia Kihoro na Foi Wambui ni watu mashuhuri nchini Kenya kwenye upande wa kidigitali na wameungana na kuweza kutengeneza kipindi halisi ili kuwasaidia wapenzi waweze kuwachumbia wapenzi wao kwa njia yenye kuleta mshangao na furaha tele.

Ehe, it’s a match

Kipindi hiki kimetengenezewa Zambia ambapo mtaalam wa mapishi anawaalika watu wawili wenye mvuto baina yao kisha kuwapikia chakula na kula pamoja nyumbani kwake na baada ya hapo, waalikwa hawa huamua kama wataendelea kukutana tena baada ya pale. Je, wawili hawa watafanikiwa kuwa wapenzi au laa?

HONEY inapatikana kuanzia kifurushi cha Compact, Compact Plus na Premium kuanzia leo Jumatatu 15 Februari 2021.

Chanzo: habarileo.co.tz