Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DNA ya mtoto wa Diamond kwa Mobeto gumzo upya

Mobetooooooo DNA ya mtoto wa Diamond kwa Mobeto gumzo upya

Sat, 13 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamisa Mobeto; ni staa wa muziki, uigizaji na mitindo wa Tanzania ambaye Oktoba 2020 alithibitisha tetesi za mzazi mwenzake, Diamond Platnumz kuchukua vipimo vya DNA na mwanawe Dylan baada ya maneno kuzidi kusambaa juu ya mtoto kuwa ni wa msanii Jaguar wa Kenya.

Mjadala huu umerudi upya baada ya Hamisa kuondoa utambulisho wa Diamond kwenye jina la mtoto huyo baada ya kudaiwa kumtelekeza siku ya birthday yake, Agosti 8, mwaka huu.

Katika majibu yake ya Oktoba, 2020, ni kweli yeye na Diamond walifanya vipimo vya DNA hivyo ili kujihakikishia na majibu yalitoka asilimia 100% mtoto huyo ni wa Diamond.

Hamisa alisema; “Tulikwenda hospitalini na tukachukuliwa vipimo vinnevinne, wakasema tusubirie wiki mbili au tatu na majibu yakatoka mtoto kwa asilimia zote 100% ni wa Diamond…”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live