Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DMX kurudi jela baada ya vipimo kuonyesha bado anatumia dawa za kulevya

2339 Dmx31 TZW

Wed, 31 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

DMX haionekani kubadilika, Rapa huyo alipelekwa katika mahakama ya Manhattan Jumanne asubuhi baada ya vipimo kuonyesha kwamba bado anatumia madawa ya kulevya na tendo hilo lilikuwa ukiukaji wa masharti yake ya majaribio.



Rapa huyo amekuwa akijaribiwa katika kesi yake ya ukimbiaji kodi. Alikuwa amekwisha shtakiwa katika kesi moja mwezi Novemba mwaka jana na alihukumiwa miaka 5 jela chini ya miaka 40 ya awali. Uamuzi umepangwa kufanyika Machi 29 mwaka huu. DMX aliamuriwa kuitumikia jela baada ya kupimwana kukutwa bado anatumia cocaine na oxycodone.

DMX alitakiwa kwenda rehab wakati alipokuwa nje ya dhamana. Mahakama ilimruhusu rapa huyo kusafiri kwa ajili ya matamasha. Mwanasheria wa DMX Murray Richman aliiambia TMZ kuwa “Nina huzuni sana ila tunahitaji kukabiliana nayo kwa usahihi. Aliongezea kuwa watakuwa wakijaribu kumrudisha DMX katika programu ya rehab.



Na <strong>Raheem Rajuu

Chanzo: bongo5.com