Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DJ Stivie azidi kumkingia kifua Diddy

Stevie J Diddy.png DJ Stivie azidi kumkingia kifua Diddy

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya nyaraka za kesi zilizofunguliwa na mtayarishaji Rodney Jones dhidi ya Diddy zikidai kuwa Party zinazofanyika nyumbani kwa Combs zimekuwa zikijikita katika biashara ya ngono, sasa Dj na producer Stivie J amekanusha suala hilo kwa kuposti video ya party inavyokuwa kwa #Diddy.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Dj #StevieJ ame-share video hiyo ya moja ya party ambazo zinafanyika nyumbani kwa #Diddy kila mwaka ikiambatana na ujumbe usemao “Hivi ndivyo Diddy Party halisi inavyoonekana”.

Ikumbukwe kuwa wiki moja iliyopita makazi ya nyota wa muziki wa hip-hop, #Sean "Diddy" #Combs, ya Los Angeles na Miami, ambapo ndiyo hufanyika sherehe hizo yalifanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.

.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live