Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DJ Khaled, Jay -Z kupanda jukwaa moja tuzo za Grammy?

Jay Z And Dj Kheled Grammy DJ Khaled, Jay -Z

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Februari 5, 2023 itakuwa ni siku ya utoaji tuzo za GRAMMY na hawa ndio Mastaa waliothibitishwa kutoa Burudani Usiku huo, Bad Bunny, MaryJBlige, Brandi Carlile, Luke Combs, Steve Lacy, Lizzo, Kim Petras, na Sam Smith.

Licha ya orodha hiyo, jarida la Variety limeripoti uwepo wa tetesi za kuwapandisha jukwaani rapa mkongwe JAY-Z na bingwa DJ Khaled ambao wanawania tuzo ya wimbo Bora wa Mwaka kupitia Collabo yao ya "GOD DID".

Tukio hilo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki kutokana na ukweli kwamba JAY-Z alitofautiana na waandaji wa Tuzo za GRAMMY baada ya kunyimwa Tuzo katika vipengele vyote 8 alivyokuwa akiwania Mwaka 2018.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live